
Ukweli Kitu Adimu, Katika Hii Dunia …
Ukweli Japo Muhimu, Watu Wanauchukia …
Ukweli Watia Hamu, Kutaka Kuusemea …
Ukweli Waleta Hofu, Sababu Unaumiza …
Ukweli Pia Amani, Tajaa Na Kufurika,
Ukweli Si Kisirani, Uhasidi Tatoweka,
Ukweli Si Uhaini, Bali Haki Kuiweka,
Ukweli Iwe Ibada, Ingawa Unaumiza.
Ukweli Japo Muhimu, Watu Wanauchukia …
Ukweli Watia Hamu, Kutaka Kuusemea …
Ukweli Waleta Hofu, Sababu Unaumiza …
Ukweli Pia Amani, Tajaa Na Kufurika,
Ukweli Si Kisirani, Uhasidi Tatoweka,
Ukweli Si Uhaini, Bali Haki Kuiweka,
Ukweli Iwe Ibada, Ingawa Unaumiza.
No comments:
Post a Comment